Kuech Deng Atem mwenye umri wa miaka 26 anasema kuwa matumaini yake ni kuwarai wapiganaji kuweka silaha chini kupitia vichekesho vyake, kwa kuwa mara nyingi wanatumia uwezo wao kupora mali na fedha kutoka kwa raiya.
Atem ambaye jina lake la kisanii ni Wokii Jeesh Commando, aliandikishwa kuwa mpiganaji akiwa na umri wa miaka 10.Yeye na watoto wenzake walipata mafunzo kwenye kambi za Aweil na Mapel na kisha baadaye kujiunga kwenye mapigano huko Heglig na Abyei mwaka 2012.
Anasema kwamba mwanzoni walitwikwa jukumu la kuwauguza wanajeshi waliojeruhiwa pamoja na kubeba silaha. Mwaka 2008, mama yake alimfuata huko Mapel na kisha kurudi naye Juba ambako alianza tena masomo.