Rais wa sasa Muhammadu Buhari anaondoka madarakani baada ya kuhudumu mihula miwili.
Vyama vya kisiasa vya Nigeria vinatakiwa kuasilisha majina ya wagombea wa urais kwa tume ya uchaguzi ifikapo June taerehe 3.
Kampeni zimepangiwa kuanza mwezi Septemba.
Makam wa rais wa sasa Yemi Osinbajo na aliyekuwa gavana wa mji wa Lagos Asiwaju Bola Tinubu ndio washindani wakuu katika kinyang’anyiro cha urais.
Uchaguzi wa mchujo kwa magavana na wabunge umepangiwa kufanyika kati ya taerehe 18 na 24 mwezi May.