Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 13:47

Mchakato wa kurekebisha upya deni la Zambia utakuwa mgumu bila mpango wa IMF -Musokotwane


Waziri wa Fedha wa Zambia Musokotwane akiwahutubia washiriki wakati wa uzinduzi wa IPO wa Mgodi wa Shaba wa Konkola Zambia katika mji mkuu Lusaka.
Waziri wa Fedha wa Zambia Musokotwane akiwahutubia washiriki wakati wa uzinduzi wa IPO wa Mgodi wa Shaba wa Konkola Zambia katika mji mkuu Lusaka.

Mchakato wa kurekebisha upya deni la Zambia utakuwa mgumu kufanikishwa  bila mpango wa IMF, Waziri wa Fedha Situmbeko Musokotwane alisema leo  Ijumaa, alipothibitisha China na wenye dhamana watajiunga katika mashauriano.

Musokotwane aliwaambia waandishi wa habari kwamba alitarajia mpango wa ufadhili wa Shirika la Fedha la Kimataifa utakamilika mwishoni mwa Juni, na Benki ya Dunia pia imejitolea kutoa rasilimali za kifedha kwa nchi mara tu makubaliano ya IMF yatakapofikiwa.

Mwaka wa 2020, Zambia ilikuwa nchi ya kwanza kushindwa kulipa deni lake wakati wa janga hili, ikipambana na mzigo wa madeni wa karibu dola bilioni 32, karibu asilimia 120 ya pato lake la ndani.

Wadai wa nchi lazima sasa wakae pamoja ili kukubaliana juu ya msamaha wa deni watakaotoa, Musokotwane alisema.

XS
SM
MD
LG