Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:47

Mchagueni Hussein Mwinyi, Magufuli awaasa Wazanzibari


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa wananchi wa Zanzibar kumchagua Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar badala ya kuchagua mgombea wa chama cha upinzani ambaye bila kumtaja jina, rais Magufuli amesema ni mzee na amekuwa akigombea kila mara na anashindwa.

Magufuli amesema hayo Jumamosi, Julai 11, 2020 katikahotuba yake ya kukubali uteuzi mara baada ya kuchaguliwa kwa kishindo. Magufuli alichaguliwa kwa kura 1,822 (asilimia 100) anaingia katika kinyang’anyrio cha urais kwa tiketi ya CCM kuwania tean urais wa Tanzania na Dkt. Mwinyi amepitishwa na chama hicho kuwania urais wa Zanzibar.

“Hussein Mwinyi namzidi umri, kanichagulieni huyu na mimi nitajisikia raha, sio mkanichagulie mtu ambaye nikifika Zanzibar nitamuambia Shikamoo, inachosha, msinichagulie shikamoo mtanipa taabu, nichagulieni huyu nitampa nguvu zote kwa kuwa ni Mdogo wangu.

Hussein Mwinyi ni mnyenyekevu sana, hajaubeba urais wa baba yake, na ndio maana wakati anashukuru hapa hajaanza kumshukuru baba yake, kamshukuru Mkapa, akamshukuru Kikwete kisha kanishukuru mimi akafuata baba yake, Mwinyi ana hekima.

“Nawaambia hii siri, Hussein Mwinyi nilimteua kuwa mgombea mwenza pamoja na Mama Samia, lakini kwakuwa Mama Samia ni mwanamke akashinda kuwa makamu wa rais, maana huwezi kushindana na Wanawake ukashinda, wanawake wanatuzidi kwa mambo mengi, wanawake oyee”

“Kama atachaguliwa Mwinyi, tutayaona matokeo, nawaomba wazanzibari acheni mambo ya upemba na uunguja, ukaskazini wala ukusini na muwe na Zanzibar yenye maendeleo.

“Nitoe wito kwa wyama vya siasa tusiwe na Wagombea hao hao, tubadilishe sampuli, sio kila siku watu walewale, mungu hajakuumba wewe tu kwamba uwe kiongozi kila siku, tuwaachie wengine, mzee Kikwete angeweza kuendelea kuwa mwenyekiti ila aliniachia na waliotangulia walifanya hivyo hivyo,” amesema Magufuli.

XS
SM
MD
LG