Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 04:32

Kiongozi wa baraza la seneti ampongeza Biden


Kiongozi wa baraza la Seneti Marekani Mrepublikan Mitch McConnell akizungumza na waandishi wa habari huko Capitol hill mjini Washington, Dec. 8. 2020.
Kiongozi wa baraza la Seneti Marekani Mrepublikan Mitch McConnell akizungumza na waandishi wa habari huko Capitol hill mjini Washington, Dec. 8. 2020.

Wiki sita baada ya uchaguzi wa rais wa Marekani, Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Mitch McConnell alikiri Jumanne kuwa Mdemokrat Joe Biden ndiye rais mteule wa nchi hiyo.

McConnell alimpongeza Biden wakati Rais Donald Trump akiendelea na madai yake yasio na msingi kwamba ameshindwa kutokana na wizi wa kura .

McConnell, ambaye alikuwa amegoma kumtangaza Biden mshindi, alisema katika hotuba ya Seneti kwamba ushindi wa Biden wa kura za wajumbe 306-232 wa Jumatatu ulimhakikishia kuwa ni mshindi wa kweli kwa miaka minne katika Ikulu ya Marekani.

Alisema kuanzia asubuhi hii , nchi yetu ina rais mteule rasmi na makamu wa rais mteule”. "Mamilioni yetu wengi tulitarajia matokeo tofauti ya uchaguzi wa rais. Lakini mfumo wetu wa serikali una michakato ya kuamua ni nani ataapishwa Januari 20.Wajumbe wa Uchaguzi wamezungumza."aliongeza McConell.

"Wamarekani wanaweza kujivunia taifa letu lina makamu rais mwanamke mteule kwa mara ya kwanza" -McConell

Kwa hivyo leo, ninataka kumpongeza Rais Mteule Joe Biden," McConnell alisema. “Rais mteule si mgeni katika baraza la Seneti. Amejitolea kwa utumishi wa umma kwa miaka mingi. Ninataka pia kumpongeza makamu wa rais mteule, mwenzetu kutoka California, Seneta Kamala Harris. "Wamarekani wote wanaweza kujivunia kuwa taifa letu lina makamu wa rais mwanamke mteule kwa mara ya kwanza kabisa." Alisema Mcconell.

Imetayarishwa na na Sunday Shomari, VOA , Washington DC

XS
SM
MD
LG