Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:56

MCC yachangia dola milioni 504 ili kuboresha usafiri kati ya Benin na Niger


Wakaazi wanapanda mitumbwi katika barabara ya jiji iliyofurika na mfereji wa maji unaofurika, katika kitongoji cha Saint Martin cha Cotonou, Benin Oktoba 9,2010.
Wakaazi wanapanda mitumbwi katika barabara ya jiji iliyofurika na mfereji wa maji unaofurika, katika kitongoji cha Saint Martin cha Cotonou, Benin Oktoba 9,2010.

Idara ya misaada ya Marekani, Millennium Challenge Corporation, hivi karibuni iliandaa aina mpya ya misaada ili kuhamasisha muingiliano wa kiuchumi na biashara ya mpakani kati ya mataifa mawili ya kiafrika.

Makubaliano ya kwanza ambayo yalitiwa saini kati ya Niger na Benin itakuwa na uwekezaji wa mamilioni ya dola kwa miradi ya usafiri pamoja na misaada mingine.

Ikitokana na mikataba kati ya Marekani na mataifa binafsi, mkataba wa kikanda wa takriban dola milioni 504 utalenga katika kupunguza gharama za usafiri kati ya bandari ya Cotonou huko Benin na mji mkuu wa Niger, Niamey.

Lakini kuna mengi zaidi, anasema Mahmoud Bah, naibu mkuu wa Millennium Challenge Corporation, idara ya Marekani ambayo imekuwa ikitoa misaada ya kigeni kote duniani kwa takriban miongo miwili.

“Pia itajaribu kuzungumzia baadhi ya kiini cha sababu za kudhibiti rasilimali za barabara. Katika nchi zote, wamekuwa na nia ya dhati ya kuboresha ukarabati wa barabara hivyo kuna haja ya kuwepo mageuzi ya sera na kitaasisi kuhusiana na ukarabati wa barabara, michango, jinsi fedha zitakavyoingia na fedha hizo zitatumika vipi kwenye barabara ambazo zinahitaji kufanyiwa matengenezo,” amesema Bah.

Benin na Niger zitachangia dola milioni 15 kwa ajili ya miradi kadhaa.

Mkataba wa kikanda pia unalenga kutokomeza vikwazo vya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili na kupunguza uharibifu kutokana na uchelewesho, Bah anasema.

MCC awali iliwekeza jumla ya dola bilioni 1.1 huko Benin na Niger. Miradi mipya inalenga kuendelea maendeleo yaliyopatikana.

“Tuna matumaini kwamba tatuunganisha uwekezaji wa awali na huu uwekezaji mpya. Bandari ya Benin itakuwa ni mfano katika eneo hilo, shukran kwa kazi ya pamoja iliyofanywa, na hii barabara inaunganisha bandari na wateja, wakulima na wateja wa huko Niamey kwenye njia ya Cotonou ni hadithi kubwa hapa. Kwa hakika naamini kwamba muingiliano wa kikanda ni sehemu muhimu sana katika maendeleo ya bara hilo,” ameongezea Bah.

Bah hivi karibun ametokea Msujmbiji. Huko, alitia saini kile kinachoitwa “aide-memoire,” kinachobainisha nia ya dhati ya Washington na Maputo ili kuwa na mkataba baadaye mwaka huu kwa ajili ya mradi wa maeneo ya pwani nchini Msumbiji.

Msumbiji ni moja ya nchi ambazo zinakabiliwa na athari mbaya sana za hali ya hewa – asilimia 65 ya raia wa Msumbiji wanaishi kwenye maeneo ya pwani ya Msumbiji. Ina takriban kilometa 2,300 za ukanda wa pwani , na kila mwaka yanakumbwa na vimbunga vibaya sana.”

Miaka minne iliyopita, kimbunga Idai kiliuua mamia ya watu nchini Msumbiji, na kuwakosesha makazi mamilioni huko Msumbiji, Zimbabwe na Malawi katika kile ambacho Umoja wa Mataifa imekiita “moja ya majanga mabaya sana ya hali ya hewa katika historia ya Afrika.”

Ili kupata fedha nyingi kutoka MCC, nchi inahitajika kukidhi viwango vya idara hiyo katika vigezo mbali mbali kuanzia utawala mpaka uhuru wa kiuchumi.

MCC hivi karibuni iliiondoa Burkina Faso katika ufadhili baada ya jeshi kuchukua nchi.

Bah anasema, “tunapoona mapinduzi katika nchi, hasa mapinduzi ya kijeshi, hilo linatufanya tuhoji na linatuhusisha vipi sis, ni mstari mwekundu huo. Hatuwezi kwenda Bungeni na kusem, “tunaomba msaada kwa ajili ya nchi hii,” wakati ambapo ukweli ni kwamba tumeona jaribio au kukiukwa kwa katiba kulikofanywa na kundi la kijeshi.”

MCC inafanya kazi kutia saini mkataba na Sierra Leone mwaka huu ili kuisaidia katika kuendeleza sekta yake ya nishati ili kuwa ya uhakika na kuufanya umeme kuwa rahisi. Wanufaika wengine huko Afrika ni Mauritania, Togo na Gambia. Senegal inaangaliwa kuongoza katika mkataba ujao wa kikanda.

XS
SM
MD
LG