Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 00:18

Mbwa wawili wa Lady Gaga walioibiwa warejeshwa


Lady Gaga
Lady Gaga

Mbwa wawili aina ya bulldog wa Lady Gaga walioibiwa katika tukio la hatari la utekaji lililomuacha msimamizi wa wanyama hao kupigwa risasi kifuani wiki hii huko Hollywood, mbwa hao walirejeshwa kwa polisi Ijumaa na hivi sasa wameungana na mwakilishi wa muimbaji huyo wa muziki wa pop, polisi imesema.

Kurejeshwa salama kwa Koji na Gustav kumetokea saa kadhaa baada ya Gaga, ambaye alikuwa anarekodi filamu huko Rome wakati wanyama wake walipotekwa Jumatano usiku, alitoa ombi kupitia mitandao ya jamii kwa “kitendo cha ukarimu” cha kuwarudisha mbwa hao nyumbani.

Mwanamke mmoja ambaye mamlaka hazijamtambulisha kwa umma aliwafikisha mbwa hao katika Idara ya polisi ya Los Angeles wakiwa salama, na walikabidhiwa kwa wawakilishi wa mwanamuziki huyo, kwa mujibu wa msemaji wa Idara ya polisi, Afisa Mike Lopez.

Watu wawili wanaoshukiwa kuwaiba wanyama hao kwa kutumia bunduki kutoka kwa mtu aliyekuwa anawatembeza, Ryan Fischer mwenye miaka 30, hata hivyo hawajapatikana, Lopez amesema.

Mbwa wa lady Gaga
Mbwa wa lady Gaga

Katika ujumbe uliokuwa umebandikwa saa kadhaa mapema katika akaunti yake ya Twitter na Instagram, Gaga amesema “moyo wake unaugua” kufuatia wizi wa silaha na aliahidi kulipa dola laki tano iwapo mbwa watarejeshwa salama, ikiwa ni pamoja na mtu yeyote aliyewanunua au kufahamu walipo.

“Mbwa wangu wapendwa Koji na Gustav walichukuliwa eneo la Hollywood siku mbili zilizopita,” aliandika katika tangazo lake pamoja na kubandika picha za mbwa wake wawili. “Ninaomba Mungu familia yangu itarejea kuwa pamoja tena kwa kitendo cha ukarimu cha kuwarejesha mbwa hao.”

Haijajulikana mara moja iwapo mwanamke aliyewaleta mbwa hao polisi Ijumaa atapewa zawadi hiyo.

Fischer alikuwa anawatembeza mbwa watatu wa Gaga katika eneo la makazi ya watu huko Hollywood Jumatano jioni wakati gari liliposimama karibu nao na watu wawili walimlazimisha awakabidhi wanyama, polisi wamesema katika tamko lao.

Mtembezaji mbwa alipigwa risasi na mmoja wa wavamizi hao, na wakakimbia na mbwa wawili. Mbwa wa tatu alitoroka na baadae polisi walimpata.

Mwanamuziki huyo alimmiminia pongezi Fischer kwa kuhatarisha “maisha yake kwa ajili ya familia yake,” akiongeza : “Wewe ni shujaa wangu milele.”

Fischer anatarajiwa kupata nafuu kamili, familia yake imeiambia tovuti ya TMZ ya wasanii maarufu Ijumaa.

XS
SM
MD
LG