Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 18:04

Makundi yalioshambulia bunge la Marekani wameelezea matakwa ya tukio lao


Wafuasi wa Donald Trump waliposhambulia jengo la bunge Marekani, Jan. 6, 2021.
Wafuasi wa Donald Trump waliposhambulia jengo la bunge Marekani, Jan. 6, 2021.

Wanachama wa makundi ya wanamgambo ambao walihusika Januari 6 walielezea matakwa yao kwamba wanataka kulipua jengo la bunge na kuuwa wajumbe  wengi kadri iwezekanavyo kwa uhusiano wa moja kwa moja na State of the Union

Wafuasi wa Donald Trump ambao walifanya shambulizi lililopelekea vifo kwenye jengo la bunge la Marekani mwezi Januari mwaka huu walionyesha wanataka kulipua jengo hilo na kuwauwa wabunge, kaimu mkuu wa polisi wa Capitol amesema Alhamis.

Vitisho vinaonesha kuwa wenye msimamo mkali wangeweza kulilenga jengo wakati Rais Joe Biden akihutubia, kaimu mkuu wa polisi Yogananda Pittman aliwaambia wabinge wakati akitetea kuendeleza usalama wa hali ya juu kwenye jengo hilo.

Wanachama wa makundi ya wanamgambo ambao walihusika Januari 6 walielezea matakwa yao kwamba wanataka kulipua jengo la bunge na kuuwa wajumbe wengi kadri iwezekanavyo kwa uhusiano wa moja kwa moja na State of the Union, Pittman aliwaambia wanachama wa Kamati ya Matumizi katika Bunge.

XS
SM
MD
LG