Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 14:41

Mbunge wa zamani wa Somalia ahusika katika mauaji ya Mogadishu


wanajeshi wa Somalia wakiangalia mabaki ya gari lililotegwa bomu mjini Mogadishu.
wanajeshi wa Somalia wakiangalia mabaki ya gari lililotegwa bomu mjini Mogadishu.

Mbunge wa zamani katika bunge la Somalia ambaye alijiunga na taasisi ya kigaidi ya al-Shabaab mwaka 2010 ni mtu ambaye alihusika na bomu la kujitoa mhanga ambalo liliuwa watu 13 mjini Mogadishu siku ya Jumanne kwa mujibu wa kundi hilo.

Salah Nuh Ismail ambaye anafahamika kama Salah Badbado alikuwa miongoni mwa wauaji ambao wameshambulia kituo cha jeshi cha Halane, al-Shabab ilisema katika taarifa kwenye radio yake ya Andalus.

Bomu hilo lilitokea kwenye mlango mkuu wa kuingia uwanja wa ndege wa Mogadishu wakati wa asubuhi muda wenye harakati nyingi hiyo jumanne.

Mlango huo uliolengwa mara kwa mara unatumiwa na wafanyakazi ambao wanatumika kwenye uwanja huo uliopo karibu na majengo ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, ambayo yanaungana na uwanja wa ndege.

Wakazi katika eneo hilo wameripoti kusikia milipuko miwili mikubwa majira ya saa tatu asubuhi kwa saa za huko.

XS
SM
MD
LG