Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:44

Mbunge wa Somalia auwawa

Wanamgambo wa kundi la Alshabab lenye mahusiano na Alqaeda huko Somalia.
Wanamgambo wa kundi la Alshabab lenye mahusiano na Alqaeda huko Somalia.

Mashahidi wanasema mbunge mmoja wa bunge la Somalia ameuwawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu Mogadishu.

Mashahidi wanasema mbunge mmoja wa bunge la Somalia ameuwawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu Mogadishu.

Khalif Jire Warfaa aliuwawa Jumapili katika wilaya ya Hamar Wayne huko Mogadishu .

Mbunge mwingine aliyeshuhudia upigaji risasi huo aliiambia VOA kwamba watu wawili waliokuwa na silaha waliojifunika sura zao walimfyatulia risasi Warfaa wakati akitoka msikiti wa Marwaas.

Msikiti wa Marwaas upo kwenye eneo linalodhibitiwa kiasi kwa na serikali ambalo limekuwa na amani katika wiki za karibuni.

XS
SM
MD
LG