Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 20:32

Mbunge wa Marekani Anthony Weiner ajiuzulu.


Anthony Weiner akitangaza kujiuzulu.
Anthony Weiner akitangaza kujiuzulu.

Mbunge wa Marekani Anthony Weiner ajiuzulu.

Mbunge wa Marekani Anthony Weiner amejiuzulu bungeni kufuatia kashfa ya ngono kupitia mitandao ya mawasiliano.

Mdemokrat huyo alitangaza uamuzi wa kujiuzulu jana alhamisi akisema mvurugano aliosababisha umeleta ugumu kuendelea na kazi yake kwenye bunge.

Aliomba msamaha kwa kile alichokiita makosa binafsi na kwa aibu aliyosababisha.

Awali Alhamisi spika wa bunge John Boehner alisema kuwa suala la Wiener linazusha utata usiohitajika , na kwamba raia wa Marekani wanataka bunge lao kuwa makini katika maswala ya kuongeza ajira .

Weiner aliomba msamaha kwa mkewe ambaye ana mimba na ambaye ni msadizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton, wazazi wake na ndugu yake kwa aibu alioiletea familia yake.

XS
SM
MD
LG