Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 12, 2025 Local time: 06:44

Mbunge Dean Phillips wa chama cha Democratic atangaza kugombea urais


Mbunge Dean Phillips kutoka jimbo la Minnesota
Mbunge Dean Phillips kutoka jimbo la Minnesota

Mbunge wa chama cha Democratic kutoka jimbo la Minnesota Dean Phillips leo Ijumaa ametangaza kuwa atawania urais kushindana na Rais Joe Biden kwenye kinyang’anyiro hicho.

Mfanyabiashara huyo milonea alitangaza ugombea wake katika video ya dakika moja iliyochapishwa mtandaoni, akisema” Tulikabiliwa na baadhi ya changamoto, tutaboresha uchumi huu na tutaiimarisha Marekani.”

Phillips anatarajiwa kufanya kampeni nje ya ukumbi wa jimbo la New Hampshire leo jioni kabla ya kuwasilisha fomu yake ya ugombea kwa katibu wa jimbo, na kuendelea na kampeni yake kwa kusafiri na basi.

Forum

XS
SM
MD
LG