Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 08:55

Mbunge David Amess wa Uingereza auawa kwa kuchomwa kisu


Mbunge David Amess wa Uingereza ambaye aliuawa kwa kuchomwa kisu akiwa na wapiga kura
Mbunge David Amess wa Uingereza ambaye aliuawa kwa kuchomwa kisu akiwa na wapiga kura

Amess mwenye umri wa miaka 69 ni mbunge wa pili wa Uingereza kuuawa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kifo chake kimesababisha hofu na ghadhabu huku wanasiasa kutoka  pande zote  wakimsifia kama mbunge muungwana ambaye alifanya kazi yake kwa kuzingatia mahitaji ya wapiga kura wake

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza ameamuru mara moja tathmini ifanyike kwa mipango ya usalama kwa wabunge wa nchi hiyo kufuatia kuuawa siku ya Ijumaa kwa mbunge m-conservative, David Amess ambaye alichomwa kisu mara kadhaa katika shambulizi linaloshukiwa la kigaidi la kiislam wakati akikutana na wapiga kura mashariki mwa London.

Amess mwenye umri wa miaka 69 ni mbunge wa pili wa Uingereza kuuawa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kifo chake kimesababisha hofu na ghadhabu kote nchini huku wanasiasa kutoka pande zote wakimsifia kama mbunge muungwana, mwenye bidii, ambaye alifanya kazi yake kwa kuzingatia mahitaji ya wapiga kura wake.

Waziri wa mambo ya ndani, Priti Patel, ambaye aliongoza mkutano usiku kucha wa vyombo vya usalama na sheria nchini humo, Jumamosi aliamuru vikosi vyote vya polisi kutathmini mipango ya usalama kwa wabunge, kulingana na msemaji.

XS
SM
MD
LG