Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:01

Mbuga ya Virunga, DRC kufungwa


Mbuga ya Virunga iliyopo DRC
Mbuga ya Virunga iliyopo DRC

Mauaji na utekaji nyara unalazimisha kufungwa kwa mbuga ya taifa ya ya Virunga huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC kwa mwaka mzima.

Wageni hawataruhusiwa kutembelea mbuga hiyo kongwe kuwaona sokwe mwitu, nyani, tembo na wanyama wengine wa porini. Mkurugenzi wa mbuga hiyo, Emmanuel de Merode alisema Jumatatu kwamba ni wazi kuwa mbunga ya Virunga limeathiriwa na ukosefu wa usalama na tatizo hilo litaendelea kwa muda kadhaa.

Baadhi ya wanyama wanaopatikana mbuga ya Virunga
Baadhi ya wanyama wanaopatikana mbuga ya Virunga

Ili mbuga hiyo kuweza kutembelewa na wageni na kuwa salama, hatua zaidi zinahitajika kuchukuliwa zaidi ya zile zilizochukuliwa siku za nyuma. Muongozaji mbuga za wanyama aliuwawa huku watalii wawili wa Uingereza pamoja na dereva wao walitekwa nyara mwezi uliopita kwenye mbuga hiyo. Raia hao wa Uingereza na dereva wao waliachiwa huru siku mbili baadae.

Lakini mashambulizi mengine yanayofanywa na makundi yenye silaha yamesababisha vifo kwa waongozaji mbuga watano, wanajeshi wawili na raia wawili waliuwawa tangu mwezi April.

XS
SM
MD
LG