Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:46

Mbabazi aahidi kusaidia vijana katika uongozi.


 Amama Mbabazi, mgombea urais Uganda akizungumza na VOA nyumbani kwake Kololo Uganda.
Amama Mbabazi, mgombea urais Uganda akizungumza na VOA nyumbani kwake Kololo Uganda.

Kiongozi wa upinzani na mgombea huru wa vugu vugu la Go Forward Amama Mbabazi, Jumanne alifanya mahojiano maalum na Sauti ya Amerika jijini Kampala Uganda.

Mbabazi ambaye ni mtulivu na asiye na makeke anayezungumza kwa taratibu na staha alijaribu kuwatoa wasi wasi wafuasi wake na wale ambao bado hawajafanya maamuzi kamili juu ya nani wampigie kura.

Alisistiza kuwa yeye alijitoa chama tawala cha NRM na kutengana na rais Museveni si kwasababu anapinga chama hicho bali anataka mabadiliko ya uongozi nchini humo.

Akijibu hoja juu ya wakosoaji wanaosema hawaoni tofauti akiwa ndani au nje ya chama hicho tawala, Mbabazi alieleza kuwa “kwanza sisi ni watu tofauti mabadiliko yeyote ni muhimu haijalishi kama ni mabadiliko kutoka pacha mmoja hadi mwingine na kuna mifano mingi akitolea mfano "Tanzania walikuwa na rais mpya ambaye kachaguliwa kutoka chama tawala na anafanya mazuri nchini humo."

Aliongeza kueleza kwamba anafikiri kuna viongozi wanaokaa kwa muda mrefu madarakani ambao wanakuwa wanachoka na hawajitofautishi kati yao na taifa na hayo matatizo yataweza tu kisha ikiwa kutakuwa na mabadiliko ya uongozi

Kuhusu agizo la tume ya uchaguzi la kuzuia wapiga kura wasiende na kamera au simu zao na kupiga picha aliwapa moyo wapiga kura waende katika vituo na camera zao bila kujali agizo hilo.

Alisema hayo akidai kwamba tume ya uchaguzi haina mamlaka ya kupiga marufuku kamera au simu na hawana msingi wowote wa kufanya hivyo, na kuuliza je wanaficha kitu gani?

Kampeni zimemalizika jana na sasa ni wakati wa tume ya uchaguzi nchini humo kuzungumzia ilivyojipanga kabla ya upigaji kura hapo kesho.

XS
SM
MD
LG