Wataalamu wa siasa za ukanda huo wanasema maslahi hayo ni katika kuweka kikomo uhuru wa Wakurdi wa Syria.
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu alisema mazungumzo zaidi yamepangwa kufanyika baadaye mwezi huu.
Wachambuzi waliozungumza na VOA wanaamini kwamba ikiwa mchakato huo utasonga mbele, mkutano wa Erdogan na Assad unaweza kuwa kufanyika.
Lakini wanatahadharisha kuwa kiongozi wa Syria Bashar al-Assad huenda hataki kumkabidhi Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan zawadi ya kisiasa kabla ya uchaguzi nchini Uturuki, ikiwezekana mwezi Mei.
Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar na mkuu wa ujasusi Hakan Fidan walikutana na wenzao wa Syria Jumatano iliyopita Moscow.
Facebook Forum