Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 16:03

Mazungumzo ya ulipaji kodi wagombea urais Marekani yashika kasi


Wagombea urais Marekani, Donald Trump (L) na Hillary Clinton.
Wagombea urais Marekani, Donald Trump (L) na Hillary Clinton.

Mazungumzo ya ulipaji kodi nchini Marekani kwa wagombea urais yamekuwa gumzo kubwa. Huku mgombea wa Republican Donald trump, akiwa bado hajatoa nakala zake za kodi licha ya sehemu ya nakala zilizovuja zinazoaminika kuwa za mwaka 1995.

Mpinzani wake wa Democratic Hillary Clinton alitoa nakala zake za kodi mwaka 2015 ikionesha mapato jumla ya dola milioni 10.7 alizotengeneza na mume wake, Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton.

Kila mgombea urais Marekani hutakiwa kuonesha nakala zake anazolipa kodi bila kulazimishwa na sio tu kwa Trump, ni utaratibu tangu mwaka 1976. Wapigakura wa Marekani wanatakiwa kuwajua wagombea wao wa urais kupitia namna wanavyolipa kodi za mapato kila mwaka hapa nchini. Alisema mchambuzi wa kisiasa John Hudak wa taasisi ya Brookings iliyopo mjini Washington.

Aliendelea kusema utaratibu huu unamsaidia mpiga kura kufahamu ni kiasi gani cha mapato mgombea anatengeneza, mapato hayo yanatoka wapi na ikibidi kuelezea aina ya biashara anayojihusisha nayo mgombea huyo. Rais barack Obama anatoa nakala zake za malipo ya kodi kila mwaka katika kipindi chake cha urais ikionesha mapato yakitofautiana kutoka dola 447,000 hadi milioni 5.6. Mapato yake mwaka 2007 ambapo nakala yake ya kodi ya mapato ilijazwa mwaka 2008 wakati alipokuwa akifanya kampeni za kuingia White House ilionesha kwamba yeye na mkewe Michele Obama walikuwa na mapato jumla ya dola milioni 4.2 ambapo fedha nyingi zilitokana na uuzaji wa vitabu alivyoandika Rais Obama.

Mpinzani wa Rais Obama wakati huo, seneta John McCain wa Republican alitoa nakala zake za kodi ikionesha mapato jumla ya dola 400,000.

XS
SM
MD
LG