Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 10:07

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa akutana na upinzani wa Syria


Staffan de Mistura, Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria

Upinzani wa Syria unasema majadiliano ya jana yametia moyo na kuonyesha dalili nzuri hasa katika masuala ya kibinadamu ambayo kundi hilo limetaka kusitishwa kwa mashambulizi ya anga kwa raia.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura leo anakutana tena na wajumbe wa upinzani mjini Geneva baada ya kupiga hatua katika kutatua baadhi ya masuala makuu waliyotaka yazungumziwe kabla ya kushiriki kwenye mazungumzo ya Amani.

De Mistura pia amepanga kukutana na maafisa wa serikali baadaye hii leo kuzungumza, lakini kwanza afanye mazungumzo na upinzani. Amesema jana Jumapili kwamba ana imani kuwa upinzani utajiunga katika utaratibu wa amani ambayo umeanza tangu Ijumaa, huku wawakilishi wa upinzani wakisusia kikao hicho katika siku ya kwanza.

Msemaji wa upinzani wa Syria amesema majadiliano ya jana yametia moyo na kuonyesha njia nzuri hasa katika masuala ya kibinadamu ambayo kundi hilo limetaka kusitishwa kwa mashambulizi ya anga kwa raia.

XS
SM
MD
LG