Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:10

Israel na Palestina kufanya mazungumzo ya amani


Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry na mwenzake wa ufaransa Jean Marc Ayrault katika picha
Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry na mwenzake wa ufaransa Jean Marc Ayrault katika picha

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, anakutana na wanadiplomasia wa ngazi za juu wa Ulaya na Mataifa ya Kiarabu leo Ijumaa, wakiwa na matumaini ya kupata uwiano, na kufufua mazungumzo ya kutafuta amani yaliyositishwa kati ya Israeli na Palestina.

Katika hotuba yake ya kufungua mkutano huo, Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, alizitaka Israeli na Palestina kuonyesha kile alichokiita “ujasiri katika kuchagua amani.”

Alisema mazungumzo kuhusu vikwazo vya kuleta azimio la kudumu kati ya Israeli na Palestina ni lazima yatilie maanani eneo lote.

Hollande aliendelea kusema kwamba mataifa yenye nguvu ulimwenguni yana jukumu muhimu la kuchangia hali ya amani kati ya Palestina na Israeli, lakini akaongeza kwamba mwishowe, itakuwa ni wajibu wa pande mbili zinazozozana kutafuta suluhisho kwa tofauti zao.

XS
SM
MD
LG