Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 11:35

Mazungumzo ya kutafuta amani Burundi yaanza Arusha


Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa Benjamin Mkapa
Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa Benjamin Mkapa

Akizungumza wakati akifungua mjadala wa mazungumzo hayo rais mstaafu bwana mkapa amesisistiza umuhimu wa pande zinazopingana kutoa ushirikiano ili lengo la kurejesha amani nchini burundi liweze kufikiwa.

Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa ameanza mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa burundi kwa kuzitaka pande zinazopingana kutambua kwamba hatima ya amani ya nchi iko mikononi mwao.

Akizungumza wakati akifungua mjadala wa mazungumzo hayo huko Arusha nchini Tanzania, rais mstaafu bwana Mkapa amesisistiza umuhimu wa pande zinazopingana kutoa ushirikiano ili lengo la kurejesha amani nchini Burundi liweze kufikiwa.

Hatua ya kuanza mazungumzo hayo imepokelewa kwa matumaini makubwa na wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa akiwemo Jamar Bonomaar kutoka umoja wa mataifa na katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki balozi Liberate Mfumukeko ambao wamesema watahakikisha kuwa wanatoa ushirikiano mkubwa.

Hata hivyo katibu wa chama cha CNDD bwana William Munyembabazi na mtendaji mkuu wa chama cha wanasheria wa Afrika wamesema hatua ya baadhi ya vyama vidogo vya upinzani na wanaharakati wengine wa Burundi kutoalikwa katika mjadala huo inaweza kuathiri mazungumzo hayo.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuendelea kwa siku nne mfululizo .

XS
SM
MD
LG