Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 07:22

UN yaomba sitisho la mapigano litekelezwe Syria kabla ya mazungumzo


Picha inamuonyesha mwanamme akiwa amembeba mtoto baada ya shambulizi la anga huko Aleppo, Syria, Alhamisi April 28.

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria amesema ananuia kufanya duru nyingine ya mazungumzo ya amani mwezi ujao, lakini ametoa wito kuwepo kwa sitisho la mapigano kabla ya kutangazwa kwa tarehe ya mazungumzo hayo.

Staffan De Mistura ameyasema haya leo Alhamisi baada ya kutoa taarifa kuhusu mazungumzo hayo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Alisema majadiliano hayo yameleta mafanikio licha ya ghasia kusambaa kwa ghasia nchini syria.

Ghasia hizo ni pamoja na shambulizi jipya kwenye hospitali iliyopo Aleppo ambalo limetokea Jumatano usiku na kuua takriban watu 20, wakiwemo wafanyakazi watatu wa hospitali. Ripoti kutoka eneo la tukio zimesema mmoja wa waathirika alikuwa ndiyo daktari pekee wa watoto aliyekuwepo katika eneo hilo linaloshikiliwa na waasi na mwingine alikuwa mtoto mdogo.

XS
SM
MD
LG