Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 08:41

Mazungumzo ya amani Jamuhuri ya Afrika ya kati yamalizika bila kupiga hatua madhubuti.


Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya kati Faustin Archange Touadera akiwasili kwenye mkutano wa chama cha MCU kwenye uwanja wa michezo mjini Bangui. Machi 18, 2022. Picha ya AFP.
Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya kati Faustin Archange Touadera akiwasili kwenye mkutano wa chama cha MCU kwenye uwanja wa michezo mjini Bangui. Machi 18, 2022. Picha ya AFP.

Mazungumzo ya amani nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati ambapo vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipamba moto tangu mwaka wa 2013, yamemalizika Jumapili bila kupiga hatua madhubuti.

Mazungumzo yalianza Jumatatu wiki iliyopita, lakini hakuna makundi ya waasi yaliyoalikwa kwenye mazungumzo hayo, na upinzani uliyasusia.

Rais Faustin Archange Touadera aliahidi mwishoni mwa mwaka wa 2020, baada ya kuchaguliwa kwa muhula mwengine katika uchaguzi wenye utata kwamba ataanda mjadala wa kitaifa kwa ajili ya maridhiano.

Ulikuwa mshangao mkubwa alipotangaza hapo tarehe 15 Machi kwamba mazungumzo yataanza na upinzani na mashirika ya kiraia tarehe 21 Machi.

Lakini ajenda ya mazungumzo haikuwa wazi na haikuwa na malengo madhubuti.

Wataalamu wa kikanda wanasema kongamano la mjadala huo lilionekana kama jaribio la kutuliza moyo jumuia ya kimataifa, ambayo imeiweka Jamuhuri ya Afrika ya kati, mojawapo ya mataifa maskini zaidi duniani, kwenye orodha ya nchi zinazohitaji msaada wa afueni.

Kulikuwa na hali ya mvutano wakati wa mazungumzo ya wiki iliyopita yaliyofanyika katika bunge la taifa mjini Bangui, hasa wakati kulipendekezwa marekebisho ya katiba yanayomrushu rais kuwania muhula wa tatu yaliyoibuwa katika majadiliano ya awali.

Pendekezo hilo liliondolewa baadaye.

Wakati wa sherehe ya kukamilisha mazungumzo, mwenyekiti wa mjadala huo Richard Filkota alitangaza kwamba mapendekezo 600 yalitolewa.

XS
SM
MD
LG