Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 01:22

Mazungumzo kuhusu bwawa la Ethiopia ‘yavunjika’


Bwawa la Grand Renaissance la Ethiopia.
Bwawa la Grand Renaissance la Ethiopia.

Misri ilisema Jumanne kwamba imeamua kujiondoa kwa mazungumzo na Ethiopia kuhusu bwawa kubwa la kuzalisha umeme ambalo ujenzi wake umegharimu mabilioni ya dola kwenye mto Blue Nile.

Misri imesema kwamba itafanya majadiliano ya ndani baada ya Ethiopia kutoa mapendekezo mapya, kuhusu namna ya kujaza bwawa hilo lililoibua utata.

Wizara ya unyunyuziaji ya Sudan imesema kwamba msimamo wa sasa wa Ethiopia umesababisha hofu namna mazungumzo hayo yanastahili kuendeshwa.

“Tunasisitiza kuhusu hatari iliyopo kutokana na ujenzi wa bwawa hilo na watu wa Sudan, ikiwemo hatari kwa mazingira na kwa jamii, pamoja na usalama wa mamilioni ya watu wanaoishi kando mwa mto Nile,” ilisema taarifa ya wizara ya unyunyuziaji ya Sudan.

Bwawa hilo la grand Renaissance, ambalo limejengwa kilomita 15 kutoka mpaka wa Ethiopia na Sudan, limesababisha mgogoro kati ya nchi hizo tatu.

Misri ina hofu kwamba mradi huo wa dola bilioni 4 unaweza kusababisha hali ya kupungua kwa maji kwa ajili ya kilimo na matumizi ya kawaida nchini Misri huku Sudan ikiwa na hofu kuhusu usalama wa watu wake, kutokana na bwawa hilo.

Misri inategemea mto Nile kwa asilimia 90 ya maji kwa ajili ya matumizi ya shughuli zake.

Nchi hiyo imesema kwamba Ethiopia imewasilisha mapendekezo ya kuendesha bwawa hilo bila kuwepo “mpango maalum” wa “kisheria wa namna ya kusuluhisha migogoro”.

Waziri wa unyunyuziaji wa Ethiopia Seleshi Bekele alikuwa ameeleza matumaini ya kupatikana mafanikio kwenye mazungumzo hayo na alikuwa ameandika ujumbe wa Twitter awali, akisema “Ethiopia ingependa kusaini mkataba wa kujaza bwawa hilo haraka iwezekanavyo na kuendelea na mazungumzo ili kukamilisha mkataba mpana.”

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema mwezi Julai kwamba nchi yake imeshajaza nusu ya bwawa hilo kutokana na mvua kubwa.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG