Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, anasema Washington na Beijing watatekeleza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini kutokana na mipango yake ya nyuklia na makombora ya masafa ya mbali.
Lakini, licha ya tamko hilo, China na Marekani zinaendelea kutokubaliana kuhusu visiwa ambavyo China inadai kuimiliki katika bahari ya “South China.”
Bwana Kerry amewaeleza wanahabari mwishoni mwa mkutano wa nane wa mwaka wa mazungumzo ya mkakati wa usalama na uchumi baina ya Marekani na China kwamba hakuna taifa lolote kati ya hayo ambalo litakubali Korea Kaskazini kuwa taifa lenye nguvu za nyuklia.
China, ambayo ni mshirika mkuu na nchi inayoinufaisha Korea Kaskazini, inaunga mkono vikwazo vikali dhidi ya Pyongyang.
Wakati huo huo, Kerry ametoa wito kwa mataifa yote yanaoyodai sehemu ya ardhi ya South China Sea kuwa wastahmilivu na kutanzua matatizo yao kupitia majadiliano na diplomasia.