Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, hafla hiyo imefanyika wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru ambapo siku kama hii mwaka wa 1960 . taifa hilo lilijipatia uhuru wake kutoka Ubelgiji.
Lumumba anakumbukwa kama shujaa wa kitaifa aliyesaidia kumaliza utawala wa kikoloni. Lumumba alifanyika waziri mkuu wa Congo baada ya uhuru lakini akauwawa kabla ya kumaliza mwaka mmoja madarakani mwaka wa 1961.
Mazishi ya Alhamisi yamefanyika baada ya Ubelgiji kurejesha mabaki yake nchini mapema mwezi huu. Jeneza lililokuwa na jino lake awali lilipelekwa kwenye sehemu tofauti za nchi , ili kutoa nafasi kwa wananchi kutoa heshima zao kikiwemo kijiji alikozaliwa cha Onalua,kilichoko kwenye jimbo la Sankuru.