Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 01, 2024 Local time: 23:29

Mawaziri zaidi wajiuzulu Tunisia


Waziri wa maendeleo, Ahmed Nejib Chebbi (kushoto).
Waziri wa maendeleo, Ahmed Nejib Chebbi (kushoto).

Mawaziri wawili akiwemo kiongozi wa upinzani wajiuzulu katika serikali ya muda ya Tunisia.

Mawaziri wawili zaidi akiwemo muanzilishi wa chama cha upinzani, wamejiuzulu kutoka kwenye serikali ya muda ya Tunisia kufuatia wiki kadhaa za maandamano dhidi ya utawala wa muda.

Ahmed nejib chebbi, muanzilishi wa chama cha upinzani cha democratic progressive, alitangaza kuondoka katika serikali hapo jana , ambapo alikuwa akishikilia wadhifa wa waziri wa maendeleo. Alielezea kutoridhishwa na mwelekeo wa serikali ya muda. Chebbi na viongozi wengine maarufu wa upinzani walijiunga katika serikali ya muda baada ya kung’olewa mamlakani mwezi January rais wa muda mrefu Zine el Abidine Ben Ali kama sehemu ya juhudi za kuisukuma mbele nchini kuelekea kwenye demokrasia.

Waziri wa elimu ya juu, Ahmed Ibrahim pia aliondoka kwenye serikali hapo jana. Anaongoza chama che Etaajdid. Siku ya jumatatu shirika rasmi la habari la nchi hiyo lilitangaza kuondoka kwa mawaziri wa mipango na teknolojia.

Waziri mkuu Mohammed Ganouchi alijiuzulu jumapili, siku moja baada ya mapambano dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali na kusababisha vifo vya watu watatu. Waandamanaji waliikosoa serikali ya muda wakisema ilikuwa inakaribiana na serikali ya zamani ya Bwana Ben Ali.

Pia hapo jana kundi la kutetea haki za binadamu la Amnesty International liliitaka serikali ya muda ya Tunisia kuchunguza matukio ya ghasia na kuhakikisha kuwa wahusika wa ghasia hizo wanawajibika.

XS
SM
MD
LG