Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 04:19

Mawaziri wa Ulinzi wa Marekani na India wakutana kujadili jinsi ya kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya ulinzi


Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin

Mawaziri wa ulinzi wa Marekani na India wamekutana leo Jumatatu mjini New Dehli kujadili jinsi ya kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya ulinzi, wiki chache kabla ya waziri mkuu wa India Narendra Modi kufanya ziara hapa Washington.

Waziri wa ulinzi wa India Rajnath Singh ameandika kwenye Tweeter kwamba mazungumzo na waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin yalijumuisha “maslahi ya pamoja ya ulinzi na kuimarisha ushirikiano wa usalama.”

Singh amesema “Ushirikiano wa India na Marekani ni muhimu kwa kuhakikisha kanda ya bahari ya hindi na bahari ya pacific inaendelea kua huru, wazi na lenye kufuata sheria.”

Ameongeza kuwa wanapanga kufanya kazi kwa karibu na Marekani katika Nyanja zote kwa ajili ya kuimarisha uwezo na ushirikiano wao wa ulinzi.

Waziri Austin alimpongeza Singh baada ya mkutano huo, akisema mwenzake wa India alisaidia kuandaa njia ya ushirikiano wa kina, mazoezi ya pamoja, na ushirikiano wa teknolojia kati ya nchi zao mbili.

Waziri mkuu Modi anatarajiwa kufanya ziara Marekani tarehe 22 Juni.

Forum

XS
SM
MD
LG