Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:08

Mawaziri wa ulinzi wa Australia na China wakutana,Singapore


Naibu waziri mkuu na pia waziri wa ulinzi wa Australia Richard Marles.
Naibu waziri mkuu na pia waziri wa ulinzi wa Australia Richard Marles.

Waziri wa ulinzi wa Australia Richard Marles mwishoni mwa wiki amekutana na mwenzake wa China Wei Fenghe pembezoni mwa kongamano la usalama la Shangri La, nchini Singapore.

Baada ya mkutano huo Marles ambaye aliwahi kuwa mkuu wa ujasusi alisema kwamba kuna safari ndefu kuelekea kurejesha kwa uhusiano kati ya taifa lake na China. Wachambuzi wanasema kwamba mkutano wa mawaziri hao Jumapili huenda ukaashiria mwanzo mpya wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo.

Uhusiano kati ya mataifa hayo umedorora katika miaka ya karibuni kiasi kwamba mashauriano ya mawaziri kati ya mataifa ya Indo Pacific hayajafanyika kwa zaidi ya miaka miwili. Miongoni mwa masuala yaliozua utata hapo nyuma ni madai ya Australia kwamba China iliingilia siasa zake kupitia udukuzi wa kimitandao, kuzuiliwa kwa raia wake nchini China, wakati Australia ikiipiga marufuku kampuni ya mawasiliano ya Huawei kutumia mfumo wa 5G nchini humo.

Mzozo pia uliongezeka baada ya janga la corona mwaka 2020 pale aliyekuwa waziri mkuu wa Australia Scott Morrison kudai kwamba China inahitaji kuchunguzwa kutokana na janga hilo.

XS
SM
MD
LG