Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 09:50

Mawaziri wa nishati wa EU waidhinisha mpango wa kupunguza matumizi ya gesi


 Josep Borrell, Mwakilishi Mkuu wa Mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya akiongea wakati wa mahojiano katika ofisi ya Ujumbe wa Umoja wa Ulaya.
Josep Borrell, Mwakilishi Mkuu wa Mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya akiongea wakati wa mahojiano katika ofisi ya Ujumbe wa Umoja wa Ulaya.

Mawaziri wa nishati wa Umoja wa Ulaya waliidhinisha mpango siku ya  Jumanne wa kupunguza matumizi ya gesi asilia kwa asilimia 15 ili kupunguza utegemezi wa usambazaji wa Russia.

Mkataba huo unahusisha upunguzaji wa hiari kati ya Agosti na Machi, na utaruhusu nchi wanachama kukusanya vifaa kabla ya miezi ijayo ya msimu wa baridi.

Ikiwa kutakuwa na dharura, EU inaweza kufanya kupunguzwa huko kwa lazima, ingawa kwa misamaha fulani ambayo ilikubaliwa kama sehemu ya maelewano ili kufikia makubaliano.

Makubaliano hayo pia yanakuja huku kukiwa na matarajio kwamba Russia itakata usambazaji wa gesi kwa Umoja wa Ulaya kujibu vikwazo vya Umoja huo dhidi ya Russia kwa uvamizi wake wa Ukraine.

XS
SM
MD
LG