Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:56

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Afrika magharibi kuzuru Guinea Ijumaa


Kikosi cha kijeshi lilichofanya mapinduzi Guinea chaingia mjini Conakry
Kikosi cha kijeshi lilichofanya mapinduzi Guinea chaingia mjini Conakry

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Afrika magharibi watawasili  Ijumaa nchini Guinea kutathmini hali baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo, waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Alpha Barry amesema Alhamisi.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso,Ghana,Nigeria na Togo wanafanya ziara hiyo kama wawakilishi wa jumuia ya uchumi ya mataifa ya magharibi ,ECOWAS, amesema Barry ambaye yumo kwenye ujumbe huo.

Jumatano, ECOWAS ilisimamisha Guinea kwenye uanachama wa jumuia hiyo baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Jumapili, ambapo kikosi maalum kinachoongozwa na Luteni Kanali Mamady Doumbouya kilichukua madaraka na kumkamata rais Alpha Conde,tukio ambalo limelaniwa na jumuia ya kimataifa.

Conde, mwenye umri wa miaka 83 amekuwa akikosolewa vikali kwa utawala wa kimavabu, huku darzeni ya wanaharakati wa upinzani wakikamatwa baada ya uchaguzi wenye utata uliosababisha vurugu mwaka uliopita.

Hata hivyo mapinduzi nchini humo yamesababisha hofu ya kurudi nyuma kwa demokrasia kote Afrika magharibi, ambapo watu wenye nguvu katika jeshi wanaendelea kuwa na mazoeya ya kuchukua madaraka.

Hali ya Guinea imekuwa sawa na jirani yake Mali ambayo ilishuhudiwa mapinduzi mwaka wa 2019.Taifa hilo la ukanda wa Sahel limekumbwa na mapinduzi mawili ya kijeshi tangu Agosti mwaka jana, yaliyoongozwa na Kanali Assimi Goita, ambaye pia alikuwa kamanda wa kikosi maalum.

XS
SM
MD
LG