Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 11:25

Mawaziri wa fedha wa nchi tajiri duniani hawajakubaliana kuhusu mfumuko wa bei


Mawaziri wa fedha wa nchi 20 tajiri zaidi duniani G20 wakiwa kwenye mkutano Indonesia. Picha: AP
Mawaziri wa fedha wa nchi 20 tajiri zaidi duniani G20 wakiwa kwenye mkutano Indonesia. Picha: AP

Waziri wa fedha wa Indonesia Sri Mulyani Indrawati amesemwa kwamba ni muhimu sana kwa mawaziri kutoka nchi 20 tajiri sana duniani G20, kukubaliana katika mazungumzo ya Bali, akionya kwamba iwapo hilo halitafanyika, italeta changamoto kubwa sana kwa nchi zenye kipato kidogo.

“Tisho kubwa la vita, kuongezeka kwa bei ya bidhaa, na mfumuko wa bei kote duniani, unaoweza kusababisha nchi kuingia katika madeni sio tu kwa nchi maskni bali pia zenye kipato cha kati au hata zilizoendelea. Hali hii ilikuw aimeanza kujitokeza kabla ya kutokea janga la virusi vya corona na sasa janga hilo limesababisha athari Zaidi na huenda ikawa vigumu hata kukabiliana nayo.”

Mawaziri wa fedha wa G20 wanakutana nchini Indonesia kujaribu kukubaliana namna ya kudhibithi mfumko wa bei na kuwepo upatikanaji wa chakula.

Hata hivyo, kuna hisia kali kuhusiana na vita vinavyoendelea Ukraine na ambavyo vimesababisha gharama ya maisha kupanda.

Mataifa 20 tajiri duniani ambayo yanajumulisha nchi za magharibi, yamewekewa vikwazo Russia kwa kuvamia Ukraine kivita.

China, India na Afika kusini zimesalia kimya na hazijatoa msimamo wake kuhusu vita hivyo.

Waziri wa fedha wa Indonesia Sri Mulyani, ametaka mataifa hayo kutozungumzia sana siasa na badala yake kukubaliana namna ya kupata suluhu kwa ukosefu wa chakula la mfumuko wa bei.

“Kuja kwetu hap ani hatua kubwa katika kusuluhisha tofauti zetu. Nina Imani kwamba ninaweza kuwategemea kwamba tutaendelea kuimarisha ushirikiano kati yetu katika kutatua mgogoro huu unaokumba ulimwengu. Hii ina maana kwamba mkutano wetu utakapokamilika, tutakuwa tumefikia akubaliano kuhusu tunachostahili kufanya kwa Pamoja kuoata suluhu.”

Waziri wa fedha wa Ukraine, Pamoja na mwenzake wa Russia wanatarajiwa kuhutubia mkutano huo kwa njia ya video.

XS
SM
MD
LG