Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 12:16

Mawaziri wa ASEAN watafakari hali kwenye bahari ya South China


Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa jumuiya ya mataifa ya kusini mashariki mwa Asia- ASEAN.

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa jumuia ya mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN, walijaribu bila ya kutafakari vyema kutoa taarifa ya pamoja yenye msimamo mkali kuhusiana na hali kwenye bahari ya South China lakini kulazimika baadae kuifutilia mbali. Balozi wa zamani wa Marekani kwenye Benki ya Maendeleo ya Asia, Curtis Chin, alielezea tukio hilo kama la ajabu na lililofanyika vibaya.

Chin aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba tukio hilo linasisitiza jinsi hali ilivyo tete katika bahari ya South China, na kuonyesha kazi ngumu inayoyakabili mataifa ya ASEAN katika kuungana pamoja kutanzua baadhi ya masuala muhimu yanayokumba kanda hiyo.

Mawaziri hao wa Asean wakikutana mjini YUXI katika mkoa wa YUNNAN, China walijaribu kumkosoa mwenyeji wao kwa kueleza wasi wasi wao mkubwa kuhusiana na kuongezeka kwa mvutano katika bahari ya South China.

XS
SM
MD
LG