Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 16:21

Mawasiliano yakatika Gaza


Gaza kwa mara ya tatu sasa mawasiliano yamekatika kabisa toka vita kuanza.

Kukosekana kwa mawasiliano kuliripotiwa na kundi la utetezi la NetBlocks.org, na kuthibitishwa na kampuni ya mawasiliano ya Palestina Paitel, na kufanya kuwa vigumu kupata taarifa ya hatua hiyo mpya ya kijeshi ya Israel.

Msemaji wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa kwa Palestina, Juliette Touma, ameliambia shirika la habari la Associated Pres kwamba wamekosa mawasiliano kwa kiwango kikubwa na wafanyakazi wa UNRWA.

Mapema Jumapili, ndege za Israel za kivita zilishambulia kambi mbili za wakimbizi za Gaza, na kuua takriban watu 53 na kujeruhi dazeni wamesema maafisa wa afya.

Forum

XS
SM
MD
LG