Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 03:37

Mawanaharakati wa Haki za Binadamu wa Morocco akamatwa wakati wa ziara ya Macron


Rais wa Ufaransa Emmanuel akiwa na Mfalme wa Morocco Mohammed wa 5 wakati wa ziara yake kwenye mji mkuu wa Rabat. Oktoba 29, 2024.
Rais wa Ufaransa Emmanuel akiwa na Mfalme wa Morocco Mohammed wa 5 wakati wa ziara yake kwenye mji mkuu wa Rabat. Oktoba 29, 2024.

Mwanauchumi wa Morocco ambaye anafahamika kutokana na harakati zake za kutetea haki za binadamu amezuiliwa kufuatia matamshi ya kukosoa serikali kupitia mitandao ya kijamii.

Hayo yalijiri wakati wa ziara ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye taifa hilo la Afrika Kaskazini. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, waendesha mashitaka walikamata Fouad Abdelmoumni mjini Casablanca, Jumatano na kutangaza kuwa anachunguzwa kwa tuhuma za kueneza habari za uongo pamoja na kutuhumu wengine kwa ukatili kupitia mitandao ya kijamii, shirika la habari la serikali ya Morocco limesema.

Iwapo atapatikana na hatia, huenda akapewa hukumu ya kifungo cha jela cha miaka 5 chini ya sheria za uhalifu wa mitandao. Shirika la Morocco la kutetea wafungwa wa kisisia kupitia taarifa limesema kuwa ukamataji wa Abdelmoumni ni kutokana na harakati zake za kutetea haki za binadamu. Limeongeza kusema kuwa ukamataji huo ni ishara ya kuongezeka kwa ukandamizaji dhidi ya haki za binadamu pamoja na wanaharakati wa kisiasa nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG