Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 01:15

Mawakili wakiri kosa la mlipuaji wa Boston Marathoni


Mchoro wa mahakamani ukimuonesha mtuhumiwa katika kesi hiyo, Dzhokhar Tsarnaev.

Mawakili wa utetezi wa mtuhumiwa wa shambulizi la mabomu la Boston Marathon, Dzhokhar Tsarney, wamesema mtuhumiwa alihusika na shambulizi.

Wameliambia baraza la mahakama katika keshi hiyo, kwamba mtuhumiwa alisaidia kubeba milipuko ya shambulio lililosababisha maafa mwaka 2013.

Mawakili wamedai kuwa kaka yake ndiye aliyepanga mpango huo wote.

Wakili Judy Clarke amekiri kwamba mtuhumiwa alihusika na kwa sasa anakabiliwa na adhabu ya kifo.

Mashambulizi hayo mawili yaliyoua watu watatu na kujeruhi wengine 264 katika mstari wa kumalizia mbio.

Clarke ni mmoja wa wataalam wakubwa wa kesi za adhabu ya kifo nchini Marekani, ameliambia baraza la mahakama katika siku ya kwanza ya mahakama kwamba utetezi wake haubariki kosa la Dzhokhar Tsarnev.

Lakini amesema kijana huyo alishawishiwa na kaka yake Tamerlan, kufanya shambulizi ambalo waendesha mashitaka wanasema lilifanywa kama kisasi kwa Marekani, kwa kujiingiza katika vita na nchi za kiislam.

Kaka wa mtuhumiwa huyo wa adhabu ya kifo aliuwawa katika mapambano na polisi baada ya kufanya mashambulizi hayo.

XS
SM
MD
LG