Utekaji nyara huo unasemekana kutekelezwa na watu waliokuwa wamevalia mavazi ya raia na kisha kushilikiwa na maafisa wa usalama wa Burkina Faso, mwanahabari mmoja wa AFP amesama.
Mkuu wa Baraza hilo Siaka Niamba, ameandika kwenye waraka aliowasilisha kwa wanahabari kwamba Baraza la Mawakili nchini humo lilifanya kikao maalum Februari 7, na kuamua kususia kazi februari 15 kote nchini, kama sehemu ya kutaka kuachiliwa kwa mwenzao Guy Herve Kama.
Kuna ripoti za utekaji nyara wa watu kadhaa wanaochukuliwa ni wapinzani wa utawala wa kijeshi uliochukua madaraka tangu Septemba 2022, chini ya uwongozi wa Kapteni Ibrahim Traore.
Forum