Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:09

Mauaji ya Mkongo yazua maandamano kudai haki za watu weusi Brazil


Moise Kabagambe, enzi za uhai wake mhamiaji kutoka Congo aliyeuawa kwa kupigwa huko Rio de Janeiro.
Moise Kabagambe, enzi za uhai wake mhamiaji kutoka Congo aliyeuawa kwa kupigwa huko Rio de Janeiro.

Moise alipigwa kwa dakika 15 kwenye ufukwe ulio na harakati nyingi ambapo watu hupita kila wakati na hakuna mtu yeyote aliyepiga simu polisi na kujaribu kuwatenganisha wapigaji wa Moise alisema wakili Rodrigo Mondengo wa chama cha wanasheria wa Brazil mjini Rio

Waandamanaji walikusanyika Jumamosi huko Rio de Janeiro, Sao Paulo na miji mingine ya Brazil kupinga mauaji ya mkimbizi wa Congo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alipigwa hadi kufa Januari 24 na kuzua hasira na chuki katika taifa zima.

Mjini Rio watu walikusanyika nje ya eneo hilo hilo katika kibanda cha ufukweni ambako Moise Mugenyi Kabagambe alikuwa akifanya kazi hivi karibuni huko Barra da Tijuca eneo linalojulikana kwa nyumba za gharama ya juu na maduka mengi makubwa. Njia mbili zilizo mbele ya kioski zilifunikwa na mabango yakioneysha picha za Moise.

Baadhi ya picha ziliunganishwa na sauti za malori. Moja wapo ilishikiliwa na watu zaidi ya kumi, pembeni ya picha ya kijana huyo aliyefariki, ikisomeka “Haki kwa Moise, Maisha ya watu weusi ni muhimu, Acha kutuua".

Moise alipigwa kwa dakika 15 kwenye ufukwe huo ulio na harakati nyingi ambapo watu hupita kila wakati na hakuna mtu yeyote aliyepiga simu polisi na kujaribu kuwatenganisha wapigaji wa Moise alisema wakili Rodrigo Mondengo wa chama cha wanasheria wa Brazil mjini Rio. "Hatuna shaka kwamba kama angekuwa mzungu anapigwa, basi kuna mtu angejitokeza kusaidia".

XS
SM
MD
LG