Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 10:13

Mauaji ya Imam mjini New York yalaaniwa


Watu wakusanyika eneo la mauwaji kueleza malalamiko yao dhidi ya imamu wa Queens.
Watu wakusanyika eneo la mauwaji kueleza malalamiko yao dhidi ya imamu wa Queens.

Polisi wa New York, nchini Marekani, wanamtafuta mtu aliyemuua imam na mshauri wake kwa kuwapiga risasi kwa karibu kwenye barabara mmoja walipokuwa wanatoka kwa sala asri siku ya Jumamosi.

Idara ya polisi ilitoa mchoro wa mshukiwa huyo, ambao ulionyesha mtu mwenye nywele nyeusi, aliyekuwa na ndevu na aliyevaa miwani.

Sababu ya mauaji hayo haikutangazwa lakini wanaharakati karibu na Msikiti wa Al-Furqan Jame Majid, katika mtaa wa Ozone park mji wa Queens, walikitaja kitendo hicho kama uhalifu wa chuki.

Kiongozi wa Msikiti ulio karibu wa Majid Al-Aman, ulio katika mtaa wa Brooklyn, Kobir Chowdhury, alisema kuwa kwa vyovyote vile, mauaji hayo ni uhalifu uliosababishwa na chuki na kufanywa na watu wanaochukia uislamu. Wengi wa waumini wa msikiti huo ni wakazi kutoka Bangladesh.

XS
SM
MD
LG