Stoltenberg pia amesema kwamba mashambulizi mapya makubwa ya Russia mashariki mwa Ukraine tayari yameanza kama yalivyotarajiwa, akiongezea kusema kwamba yameanza kabla ya kukamilika mwaka mmoja toka kuanza kwa mashambulizi ya Russia, Febuari 24.
Akiwa mjini Brussels, Stoltenberg aliwaambia wanahabari kwamba ni wazi kwa sasa wanakimbizana na usafirishaji wa vitu muhimu kama risasi, mafuta, na vifaa vya matengenezo ili kufika Ukraine kabla Russia haijafanikiwa katika uwanja wa mapambano.
Stoltenberg alitoa kauli hii siku moja kabla ya mkutano wa tisa wa mawaziri wa ulinzi wa NATO kwa ajili ya Ukraine, unaofahamika kama mkutano wa Ramstein, ambao unatazamiwa kufanyika katika mji mkuu wa Ubelgiji wa Brussels.