Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 20, 2025 Local time: 23:03

Matumizi ya bangi yameongezeka Marekani zaidi ya unywaji pombe


Mwanamke ambaye hakutambuliwa akivuta bangi Feb. 6, 2011.
Mwanamke ambaye hakutambuliwa akivuta bangi Feb. 6, 2011.

Utafiti mpya unaonyesha kwamba idadi ya watu wanaovuta bangi kila siku nchini Marekani ni zaidi ya watu wanaokunywa pombe.

Utafiti huo umechapishwa leo Jumatano katika jarida la uraibu wa dawa za kulevya.

Utafiti ulizingatia taaririfa za kitaifa kuhusu matumizi ya dawa na afya na kuangazia zaidi matumizi ya tumbaku, pombe na dawa za kulevya.

Hii ndio mara ya kwanza tangu mwaka 2022, utafiti unaonyesha kwamba idadi ya watu wanaovuta bangi inazidi idadi ya wale wanaokunywa pombe.

Utafiti mwingine unaonyesha kwamba watu wanaovuta sana bangi wanakabiliwa na hatari kubwa ya kuwa waraibu wa bangi na kupata madhara yanayotokana na uvutaji bangi ikiwemo kupoteza uelewa wa mambo yanayoendelea maishani.

Forum

XS
SM
MD
LG