Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 08:58

Matukio: Kabla na baada ya mauaji ya Martin Luther Jr


Kumbukumbu - Mchungaji Martin Luther King Jr. akiwa na viongozi wanaharakati wa haki za raia katika nyumba ya malazi Lorraine Motel in Memphis, Tenn., siku moja kabla ya kuuwawa katika eneo hilo hilo Aprili 3, 1968.

Martin Luther King Jr., mwanaharakati ambaye alijitolea maisha yake kupigania haki za raia nchini Marekani, aliuwawa miaka 50 iliyopita mnamo April 4, 1968. Ufuatao ni mtiririko wa matukio mbalimbali kabla na baada ya kuuwawa kwake.

April 3, 1968- King anawasili huko Memphis Tennessee, kuunga mkono kugoma kwa wafanyakazi wanaoshughulika na usafi wa mji. Anakodi chumba katika nyumba ya malazi ya Lorraine.

April 4 (kabla ya saa 6pm)- King atoka chumbani katika nyumba ya malazi kwenda kupata chakula cha usiku nyumbani kwa waziri wa eneo hilo. Wakati akisubiri nje ya chumba chake akiongea na dereva wake katika eneo la nyumba ya malazi.

April 4 (6:01 p.m) – King anarushiwa risasi na kuharakishwa Hospitali ya St Joseph

April 4 (7:05 p.m)- King anatangazwa kuwa amekufa. Machafuko yanaibuka katika miji mikuu zaidi ya 100 nchini Marekani. Rais Lyndon B. Johnson anatangaza hali ya hatari.

April 5- Shirika la Upelelezi wa makosa ya jinai (FBI) unaanza uchunguzi juu ya mauaji ya King, ambao unagharimu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 2 na kuwahusisha wachunguzi zaidi ya 3,500.

April 9- Maziko ya King yanafanyika huko katika Kanisa la Ebenezer Baptist Church mjini Atlanta, Jimbo la Georgia. Zaidi ya watu 50,000 wanashiriki katika maziko yake na jeneza lake likitembezwa mji mzima kwa gari la farasi.

Aprili 19- Uchunguzi wa Shirika la FBI unajikita juu ya jina la James Earl Ray, 40, ambaye alama zake za vidole, kwa mujibu wa wachunguzi, zilikuwa zinafanana na alama zilizopatikana katika bunduki aina ya rifle iliotumika kumuua King. Mtu ambaye alikuwa amehukumiwa tayari kwa wizi wa kutumia silaha alikuwa ametoroka jela ya Jimbo la Missouri mwaka uliopita.

Aprili 24- Ray anajipatia pasi ya kusafiria ya Canada akitumia jina la George Sneyd na kununua tiketi ya ndege kutoka Toronto akielekea London.

Juni 8- Ray anashikiliwa uwanja wa ndege wa Heathrow London baada ya kujaribu kununua tiketi ili afanye safari kuelekea Brussels na baadae kukamatwa na kurejeshwa nchini Marekani.

Machi 10, 1969- Ray akiri kosa la kumuua King na kuhukumiwa kifungo cha miaka 99 katika jela ya Tennessee.

Machi 13, 1969- Ray akanusha kosa alilokiri, akidai kuwa alilazimishwa kukiri kosa hilo. Na aliendelea kusema hana makosa hadi mwisho wa maisha yake.

1978- Ray atoa ushahidi mbele ya Kamati Teule ya Bunge juu ya mauaji, ambapo baadae inatoa majumuisho kuwa Ray alifanya uhalifu huo akiwa peke yake. Hata hivyo, kamati ilihitimisha kuwa kulikuwa na ushahidi wa mazingira ulioonyesha ushahidi wa kimazingira wa kuwepo njama za mauaji hayo.

Disemba 1993- Aliyekuwa mmiliki wa mgahawa huko Memphis Loyd Jowers anasema wanachama wa kikundi cha ujangili cha Mafia walimlipa Dola 100,000 ili apange mauaji ya King. Jowers anasema alimkodi Frank Holt, ambaye alikuwa anafanya kazi ya kibarua, kumuua King.

Aprili 23, 1998- James Earl Ray alikufa jela kutokana na maradhi ya ini na figo akiwa na umri wa miaka 70.

1999- Familia ya King, ambayo inaamini Ray alikuwa hana hatia, ilimshtaki Loyd Jowers kwa kuhusika na kifo cha King. Kesi ya madai ilimalizika kwa familia hiyo ya King kulipwa dola 100, ambayo ilitoa mchango katika masuala ya hisani.

Juni 2000- Mwanasheria Mkuu wa Marekani Janet Reno alifanya uchunguzi wa nne baada ya Ray kukata rufaa, na hakuweza kugundua njama yoyote

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG