Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 22:44

Matokeo ya uchaguzi wa awali yanashangaza Marekani


Mgombea wa urais wa Marekani, Bernie Sanders.

Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura ulionesha Hillary Clinton atapata ushindi kwa urahisi jimbo la Michigan, lakini Sanders alimshinda akipata asilimia 50 ya kura.

Seneta wa Vermont Bernie Sanders amepata ushindi usiotarajiwa katika uchaguzi wa awali jana wa chama cha Demokrat katika jimbo la kaskazini la Michigan.

Kura za maoni ya wapiga kura zimeonesha kuwa waziri wa zamani wa mambo ya nje, Hillary Clinton, atapata ushindi kwa urahisi katija jimbo la Michigan, lakini Sanders alimshinda kwa asilimia 50 ya kura.

Sanders alisema ushindi wa Michigan unamaanisha mapinduzi ya kisiasa yana nguvu kote nchini na kwamba anaamini maeneo ambayo kampeni yake ina nguvu ni yale ambayo bado hayajapiga kura.

Clinton alishinda kiurahisi uchaguzi mwingine uliofanyika hiyo hiyo Jumanne katika jimbo la kusini la Mississippi.

Pia Donald Trump wa chama cha Republikan aliongeza ushindi wake katika majimbo ya Michigan, Mississippi na Hawaii.

XS
SM
MD
LG