Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:02

Matokeo ya uchaguzi Congo yameahirishwa kwa saa 48


Waunga mkono wa Tshisekedi wasema hawaamini matokeo ya uchaguzi , lakini wanasema hawataandamana mpaka kiongozi wao Etienne Tsisekedi atakapowapa maelekeza.
Waunga mkono wa Tshisekedi wasema hawaamini matokeo ya uchaguzi , lakini wanasema hawataandamana mpaka kiongozi wao Etienne Tsisekedi atakapowapa maelekeza.

Maelfu ya askari wanafanya doria katika mitaa ya mji mkuu Kinshasa wakihofia waandamanaji.

Vyombo vya habari vya serikali katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vinasema tume huru ya taifa itaahirisha kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais kwa saa 48.

Tume inasema inahitaji muda zaidi kuchanganya matokeo kutoka kila pembe ya taifa hilo la afrika ya kati.

Kuchelewa huko kutoa matokeo kamili kunaweza kuongezeka hofu ambazo tayari zinapanda juu ya uwezekano wa kuzuka ghasia za kisiasa. Maafisa walikuwa wakitegemea kutangaza mshindi kabla ya muda wa mhula wa rais Kabila kumalizika jumanne usiku.

Maelfu ya askari wanafanya doria katika mitaa ya mji mkuu Kinshasa na pia miji mingine kwa kutegemea maandamano kutokea.

XS
SM
MD
LG