Kundi la kwanza la mateka likitarajiwa kuachiliwa kutoka Gaza saa kumi jioni, kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar, ambayo inasaidia kujadili mpango huo.
Usitishaji huo wa kwanza tangu vita kuanza mwezi uliopita utajumuisha usitishaji vita wa pande zote kaskazini na kusini mwa Gaza, msemaji wa Majed Al-Ansari, aliwaambia waandishi wa habari jijini Doha.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, wanawake na watoto 50 waliotekwa nyara kutoka Israel, na kundi la wanamgambo wa Hamas Oktoba 7 wataachiliwa kwa kubadilishana na wanawake 150 wa Kipalestina na watoto wadogo waliofungwa gerezani nchini Israel.
Mateka 13 wataachiliwa kutoka Gaza, Ijumaa, na makundi mengine ya mateka yataachiliwa kila siku ya kusitisha mapigano hadi 50 waachiliwe.
Forum