Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:30

Matatizo ya kibinadamu yaongezeka jimbo la Jonglei-Umoja wa Mataifa.


Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York. (AP Photo/Osamu Honda)
Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York. (AP Photo/Osamu Honda)

Valerie Amos, naibu katibu mkuu wa masuala ya kibinadamu na mratibu wa misaada ya dharura atatembelea majimbo ya central Equatorial na Jonglei.

Umoja Mataifa unapeleka afisa mwandamizi wa masuala ya kibinadamu huko Sudan Kusini. Katika taarifa iliyotolewa jana, taasisi hiyo ya dunia imetangaza kwamba Valerie Amos, naibu katibu mkuu wa masuala ya kibinadamu na mratibu wa misaada ya dharura atatembelea majimbo ya central Equatorial na Jonglei kuanzia Jumatano hadi ijumaa. Taarifa inasema wakati wa ziara yake Sudan Kusini, Amos atakwenda mji mkuu wa Central Equatoria, Juba na atakutana na maafisa wa serikali, wafadhili na mashirika ya misaada. Umoja mataifa unasema kuongezeka kwa ghasia katika siku za karibuni kwenye jimbo la Jonglei kumesababisha matatizo ya kibinadamu ambayo tayari yalikuwepo huko Sudan Kusini.

XS
SM
MD
LG