Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:17

Mataifa yaanza kurejea hali ya kawaida baada ya janga


Mkuu wa WHO Tedros Adhanom
Mkuu wa WHO Tedros Adhanom

Wakati ulimwengu ukiendelea kujikwamua kutokana na janga la corona, baadhi ya nchi zimeanza kufungua shughuli za kawaida baada ya kuathirika kwa takriban miaka miwili.

Waziri mkuu wa jimbo la New South Wales nchini Australia Dominic Perrotte Jumatatu amesema kwamba wamejiunga na ulimwengu tena, baada ya kufungua safari za kimataifa zilizositishwa muda mfupi baada ya janga kutokea.

Israel kwa upande wake Jumapili imesema kwamba itaruhusu wasafiri wa kimataifa kuingia nchini, mradi wawe wa vipimo vya corona wanapotua au kuondoka, kuanzia Machi mosi. Kutokana na vifo pamoja na athari nyingine miongoni mwa wafanyakazi wa afya tangu janga hilo kutokea, shirika la afya duniani pamoja na shirika la kimataifa la wafanyakazi, wamechapisha mapendekezo ya kuhakikisha usalama wao wakati wa majanga. Katika miezi ya kwanza ya janga la corona, takriban wafanyakazi 115,000 wa afya wanasemekana kufa kote ulimwenguni.

Mratibu wa masuala ya wafanyakazi kwenye shirika la afya duniani James Campbell amesema Jumatatu kwamba janga la corona limefichua mapungufu yaliyopo katika kulinda usalama pamoja na maslahi ya wafanyakazi wa afya ulimwenguni. Kituo kinacho fuatilia maambukizi ya corona ulimwenguni cha Johns Hopkins kimesema Jumatatu kwamba kuna takriban maambukizi milioni 424 ya corona kote ulimwenguni pamoja na takriban vifo milioni 6 tangu janga hilo lilipozuka.

XS
SM
MD
LG