Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:40

Mataifa ya dunia yasaidia Japan


Mwanajeshi wa Marekani akisaidia katika kazi za kusafisha taka baada ya janga la tsunami katika mji wa pwani wa Misawa , Japan.
Mwanajeshi wa Marekani akisaidia katika kazi za kusafisha taka baada ya janga la tsunami katika mji wa pwani wa Misawa , Japan.

Wakati Japan inapokabiliana na maafa makubwa kutokana na mtetemeko wa ardhi mataifa yote duniani yameanza kuwasilisha misaada ya dharura.

Mtetemeko wa ardhi uloleta maafa makubwa huko Japan ulikuwa na nguvu nyingi hata kuweza kuongeza kasi za mwenedo wa dunia kwa nukta ya sekunde.

Wanasayansi wa Marekani wanasema mtetemeko huo pia umesababisha ardhi ya Japan kusonga upande wa mashariki kwa hadi mita 4.

Wakati Japan inatathmini maafa yaliyotokea mataifa kote duniani yameweka kando tofauti zao na kuanza kutoa msaada wa dharura kwa taifa hilo la kisiwa

Juhudi za msaada wa kimataifa zilianza kufika kutoka Marekani mpaka Afghanistan, kutoka kwa mashirika ya msaada na kijeshi, timu za michezo na hata watu maarufu kama vile mwimbaji Lady Gaga.

Wakati Japan inapeleka wanajeshi laki moja kuwasaidia walionusurika na janga manuari nane za kivita kutoka Marekani ziliwasili katika ufukwe wa Japan kuungana na juhudi hizo. Washington pia ilituma kundi la uokozi la watu 150 kusaidia katika eneo la tukio.

Idara ya maendeleo ya kimataifa ya Marekani, imesema imewatuma maafisa 72 pamoja na mbwa walio na mafunzo ya kutafuta binadamu, pamoja na vifaa vya uokozi.

Canada imesema inajiweka tayari kusaidia kwa chochote kinachohitajika, Australia inatuma mbwa na kundi la uokozi wakati jimbo la Kandahar, la Afghanistan ambalo limekumbwa na vita kwa miaka kadhaa linatoa msaada wa dola elfu hamsini.

Uingereza na Ufaransa kwa upande wao zinapeleka watu wenye ujuzi na kazi za uwokozi na vifaa vya dharura, wakati Japan inakabiliana na changamoto kubwa la kuwasilisha chakula na maji kwa walonusurika.

Serikali ya Moscow imeweka kando ugomvi wake wa ardhi na Tokyo na imeongeza huduma za nguvu za umeme kwa taifa hilo ambalo limeshuhudia mitango yake ya nuklia lkuharibika kutokana na mtetemeko huo mkubwa wa ardhi.

XS
SM
MD
LG