Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 03:39

Mataifa ya Afrika yanazidi kudidimiza matumizi ya mitandao


Mfano wa huduma za mitandao zinazodhibitiwa Afrika.
Mfano wa huduma za mitandao zinazodhibitiwa Afrika.

Ripoti kutoka Burundi zinasema polisi wamewakamata watu wanane siku ya Jumamosi kwa shutuma za kusambaza taarifa za kupinga serikali kwenye mtandao. Hatua hiyo ya Burundi sio jambo geni barani Afrika.

Orodha ya mataifa ya Afrika yanayojaribu kuzuia au kudhibiti mitandao ya kijamii inaongezeka hususan katika kipindi cha uchaguzi. Henry Mhina, mkurugenzi wa jarida la Article 19 la Afrika Mashariki, taasisi ambayo inatetea uhuru wa kujieleza anasema serikali katika eneo hilo bado zinadidimiza uhuru wa kujieleza.

Facebook
Facebook

Zimbabwe hivi karibuni ilianza kutumia sheria ya mwaka 2002 inayokataza kumtusi rais ili kuwakamata watu kwa taarifa walizozitoa kwenye mitandao ya kijamii.

Nchi ya Angola ilibuni “Angola Social Communication Regulatory Body” inayoendeshwa na chama tawala ili kuhakikisha inadhibiti sheria mpya ya vyombo vya habari.

Wakati huo huo mataifa mengine barani Afrika kama Mali ilifungia mitandao ya kijamii mjini Bamako mwezi wa nane kufuatia kukamatwa kwa mwandishi wa habari maarufu kwenye redio baada ya kukamtwa kwake kusababisha ghasia za waandamanaji ambapo watu kadhaa waliripotiwa kuuwawa.

Huduma mojawapo ya mitandao ya kijamii
Huduma mojawapo ya mitandao ya kijamii

Nayo serikali ya Uganda ilizuia fursa kwa mitandao ya kijamii kusambaza taarifa wakati wa uchaguzi mkuu wa urais uliofanyika Februari mwaka 2016 na tukio hilo kujirudia tena wakati wa kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwepo madarakani kwa muda mrefu nchini humo. Lakini Waganda wengi waliweza kupata taarifa za kile kinachoendelea nchini mwao kupitia mtandao binafsi au VPN.

Katika ripoti ya mwaka 2015 ya Privacy International ilielezea kwa kina matumizi ya kiupelelezi yaliofanywa na polisi na jeshi nchini Uganda ili kufuatilia wafuasi wanaoongoza upinzani, wanaharakati, maafisa waliochaguliwa, wapelelezi walioko ndani ya mfumo wa kazi pamoja na waandishi wa habari kufuatia uchaguzi wa mwaka 2011. Serikali ya Uganda ilikanusha shutuma hizo na kukataa kufanyika uchunguzi bungeni juu ya suala hilo.

XS
SM
MD
LG