Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 03:18

Mataifa ya Afrika Mashariki yaongeza matumizi


Waziri wa fedha wa Kenya Robinson Njeru Githae akiwasilisha bajeti bungeni Juni 14, 2012
Waziri wa fedha wa Kenya Robinson Njeru Githae akiwasilisha bajeti bungeni Juni 14, 2012

Mawaziri wa fedha wa Kenya Uganda Tanzania na Rwanda watangaza matarajio mazuri ya ukuwaji lakini wachambuzi watahadharisha kutokana na kuongezwa matumizi zaidi

Mawaziri wa fedha wa Kenya Uganda Tanzania na Rwanda wanakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha wanaendelea na viwango vya ukuwaji wa hivi karibuni huku wakikabiliwa na hali tete ya uchumi duniani pamoja na viwango vya juu vya ughali wa maisha na kushuka kwa sarafu zao.

Kenya yenye uchumi mkubwa katika kanda hiyo inaongeza matumizi ya bajeti yake ya 2012/2013 kwa zaidi ya asili mia 20 kufikia dola bilioni 17.10.

Tanzania imeongeza kwa asili mia 11 na kufikia dola bilioni 9.53. mawaziri wa fedha wa nchi hizo wanasema matumizi yameongezeka zaidi kwa ajili ya kugharimia uwekezaji katika ujenzi wa barabara, njia za reli na vinu vya kuzalisha umeme ili kuweza kukidhi mahitaji yanayotokana na ukuwaji wa uchumi.

Nayo Uganda taifa la tatu kwa ukubwa upande wa uchumi inaongeza matumizi yake kwa sili mia 16.7 na kufikia dola bilioni 4.49.

Rwanda bajeti yake imeongezeka na nakisi kufikia karibu asili mia 80 ambapo sehemu kubwa ni kwa ajili ya miundo mbinu pia. Na nakisi hiyo itaweza kujazwa kutokana na mikopo ya nchi za kigeni.

Wachambuzi wanasema nyongeza hizo kutasababisha nakisi katika majeti za mwaka huu na kuweza kupunguza viwango vya ukuwaji wa uchumi. Wamekosowa pia mipango ya serikali kutegemea vyanzo vya nje kupata fedha kugharimia nakisi zao.


XS
SM
MD
LG