Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:12

Mataifa takribani 50 yameahidi kusaidia wakimbizi duniani


Wahamiaji kutoka Afrika kaskazini wakiwa Athens, Ugiriki.
Wahamiaji kutoka Afrika kaskazini wakiwa Athens, Ugiriki.

Maelfu ya wahamiaji na wakimbizi wanakimbia bara la Afrika kuelekea ulaya na kwingineko baadhi wanaangalia njia mpya za kufanikisha maisha bora ya watu kwa ajili ya makazi yao kwenye bara hilo.

Zaidi ya mataifa 50 ikiwemo nchi za Marekani, Uingereza na Ulaya zimeweka ahadi ya msaada wa kifedha kuzisaidia nchi ambazo ni vyanzo vikubwa vya wakimbizi na wahamiaji. Kwa pamoja wameahidi kuongeza mchango katika mwaka huu kufikia dola bilioni 4.5 ikiwemo dola bilioni moja kutoka Marekani.

Nia hizo zilifanywa wakati wa mkutano wa viongozi juu ya wakimbizi uliomjumuisha Rais wa Marekani Barack Obama wakati wa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Nia hii ni ishara ya uwajibikaji wa kweli katika maswala ya kibinadamu ambayo yanatumika kuelezea makundi ya wakimbizi lakini hayafikii kwenye kiini kinachosababisha tatizo hili, alisema Jennifer Fenton, ofisa habari wa umma kwenye idara ya Umoja wa Mataifa ya kushughulikia wakimbizi-UNHCR.

XS
SM
MD
LG